Home Michezo Alexis Sanchez Akamilisha Uhamisho Kwenda Manchester United

Alexis Sanchez Akamilisha Uhamisho Kwenda Manchester United

by Jamhuri

Imeripotiwa kuwa mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez amefikia makubaliano na Manchester United kwa ajili ya uhamisho wa Januari.

Sanchez atakuwa amemaliza mkataba wake Emirates Stadium ifikapo mwisho wa msimu huu na Arsenal wanaaminika kuwa tayari kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile mwezi huu, hata kama ni kumuuza kwa washindani wao wa ligi.

Manchester City imekuwa timu inayopewa nafasi kwa muda mrefu kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 na kulikuwa na makubaliano baina yao majira ya joto kabla ya Arsenal kugeuza kibao, lakini United wameibuka kuwa mstari wa mbele kwa sasa.

Taarifa nyingi kwenye Twitter zimedai kuwa mchakato huo umeshakamilika, United wakita tayari kumlipa Sanchez £350,000 kwa wiki pamoja na adau ya uhamisho ya £30m.

Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger amebainisha kuwa mustakabaliwa Sanchez utafahamika ndani ya saa 48, ingawa hakuna tamko rasmi kutoka kwa klabu yoyote baina ya hizo mbili.

Sanchez alijiunga na Arsenal 2014 na amefunga mabao 80 katika mechi 165 kwa klabu hiyo.

 

You may also like