Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,Arusha

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA), imesema, kampuni za usafiri kwa njia ya mtandao Bolt na Uber zinatarajia kurejea kutoa huduma za usafiri nchini Tanzania.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu, Septemba 12, 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Habibu Suluo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.

LATRA wametoa taarifa hizo kipindi ambacho kampuni hizo kwa nyakati tofauti, walisitisha kutoa huduma za usafiri za magari na kubaki na bodaboda pamoja na bajaji.

Amesema wamesikia kilio cha kampuni hizo na wameitana kukaa meza moja kwa mazungumzo na tayari wamekubaliana kutatua tatizo ili kurejesha huduma.

“Uber walijitoa baada ya tangazo la LATRA la nauli na tiketi za mtandao ambao uliwataka kutoza tozo halali kwa amri ya kutekelezwa na wakafungua kesi Baraza la Ushindani kupinga maamuzi yetu.”

“..Bolt waliendelea kutoa huduma lakini baadae nao wakaleta taarifa kuwa wanaenda kusitisha huduma lakini tuliwaita tukiamini katika mazungumzo.

By Jamhuri