Watu 12 wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la abiria la kampuni ya Frester Iililokuwa likitoka Bukoba kwenda Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na lori lenye shehena ya saruji lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma.

Ajali hiyo imetokea saa 6 usiku wa kuamkia leo Februari 9,2023 katika Kijiji Cha Silwa Pandambili barabara kuu ya Dodoma – Morogoro huku chanzo cha ajali hiyo ikidaiwa ni dereva wa basi kutaka kulipita gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari.

Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Kamishna Awadh Haji amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kufika eneo la ajali na kutoa rai kwa madereva kuzingatia usalama na sheria za barabarani.

Katika ajali hiyo majeruhi ni 63, wanaume 40 na wanawake 23 ambao wanefikishwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Dodoma na wengine wamepelekwa Hospitali ya Gairo mkoani Morogoro.

By Jamhuri