Na Mwandishu Wetu,JamhuriMedia, Mara

Rais wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA), Bw. Paul Koy ameishauri Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), kusaidia wafanyabiashara wa mkoa wa Mara ili warasimishe biashara zao.

Kauli hiyo ameitoa jana alipotembelea banda la BRELA kwenye Maonesho ya Mara Business Expo 2022 yanayofanyika Musoma, mkoani wa Mara

“Nawaomba sana BRELA muwasaidie wafanyabiashara wa mkoa huu maana wanahitaji sana huduma zenu”, ameeleza Bw. Koy

Bw. Koy amesisitiza kuwa mbali na kutoa huduma za usajili na utoaji wa leseni kwenye banda inabidi BRELA itoe elimu kwa wananchi wanaozalisha bidhaa mbalimbali.

Kwa upande wake Afisa Leseni wa BRELA, Bw. Rajab Chambega amemhakikishia kuwa Taasisi hiyo imejipanga vema kutoa huduma kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Mara na mikoa jirani wanaotembelea maonesho hayo.

Pia ameeleza kuwa kila mfanyabiashara anayeshiriki maonesho hayo atatembelewa na kupewa ushauri na pia kusaidiwa kurasimisha biashara yake.

BRELA inashiriki kwenye Maonesho ya Mara Business Expo 2022 na kutoa huduma za usajili na utoaji wa leseni papo kwa hapo hadi tarehe 11 Septemba, 2022.

ishauri Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), kusaidia wafanyabiashara wa mkoa wa Mara ili warasimishe biashara zao.

Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 4 Septemba, 2022 alipotembelea banda la BRELA kwenye Maonesho ya Mara Business Expo 2022 yanayofanyika Musoma, mkoani wa Mara

By Jamhuri