Category: Makala
NUKUU ZA WIKI
Mwalimu Nyerere: Vyama vijihadhari kutumiwa
“Shughuli za demokrasia lazima ziwe kazi ya kudumu katika chama cha kidemokrasia na katika taifa la kidemokrasia, vinginevyo chama hicho wakati wote kitakuwa katika hatari ya kutumiwa na wakorofi wachache tu.”
Maneno haya ni ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Tujifunze uzalendo, uchapaji kazi wa Wamarekani
Mwaka 2004 nilipata fursa ya kuzuru maeneo kadhaa nchini Marekani kwa muda wa takribani mwezi mmoja. Ilikuwa ziara nzuri. Nilijifunza mengi. Wasafiri wanasema kama hujafika Marekani, hujasafiri. Kauli hii inaweza kuwa ya kweli kwa sababu kuna mengi ya kustaajabisha na kutafakarisha – kuanzia kwenye maendeleo hadi tabia zao.
Mashabiki wa upinzani wajitazame upya
Tanzania ya leo inafuata mfumo wa vyama vingi. Katikati ya mfumo wa vyama vingi Watanzania wamegawanyika katika makundi makuu matatu.
fikRA YA HEKIMA
Watanzania na imani potofu ziara ya Obama
Ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama, hapa Tanzania imenilazimu kuleta mada hii mapema tofauti na nilivyokusudia awali. Watanzania wengi wamezungumza ya moyoni mwao kuhusu ugeni huu.
FASIHI FASAHA
Haki, ukweli ni nguzo za amani – 4
Katika makala tatu zilizotangulia nimezungumzia baadhi ya viongozi wa dini, siasa na wa serikali kutupilia mbali maadili na miiko ya uongozi na kuwa chanzo cha kutaka kuvunja amani ya nchi. Pili, haki na ukweli ni nguzo za amani.
KAULI ZA WASOMAJI
Gharama KCMC zinatisha
Serikali inajitahidi kuboresha huduma kwa wananchi wenye kipato cha chini, lakini baadhi ya hospitali haziko kwa ajili ya huduma za tiba ila ni biashara tu! Ni Watanzania wangapi wanaweza kumudu gharama za sasa za KCMC kama sio kufa kwa wagonjwa?
Mtanzania mzalendo, Moshi