Chalamila atoa rai kwa viongozi wa dini kuiombea Serikali

Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Albert Chalamila, amesema Serikali inategemea maombi ya viongozi wa dini, kupitia sala na dua za viongozi wa dini na wachungaji ndipo tunapata viongozi wa Serikali wenye hofu ya Mungu.

RC Chalamila amesema hayo mapema leo Oktoba 25, 2023 katika Kongamano la Siku tatu (3) la viongozi wa duni na wachungaji wa makanisa ya Kipentekoste Mbezi Beach kwa Zena Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Albert Chalamila akiwa katika kongamano hilo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan amesema rais yuko nje ya nchi alitamani awepo na nyinyi leo, “amenituma nije kwa ajili yake anawasalimu sana pia anawatakia kongamano jema lenye mafanikio, Serikali iko pamoja nanyi” amesema Chalamila.

Aidha .kuu wa mkoa amesema kongamano hilo liwe kuchocheo cha kuwafanya viongozi wa dini na wachungaji kujiimarisha katika uinjilishaji, kuongoza kwa haki, usuluhishi na utatuzi wa migogoro, kuubiri neno na kuliishi na mengine mengi yanayofanana na hayo. ” Niwaombe wakati wote kuendelea kuiombea Serikali hasa pale inapokua na dhamira njema katika uwekezaji saa nyingine huchelewa kutafsirika vizuri kwa watu ndipo wale wenye nia ovu kwa Serikali hupata nafasi ya kupotosha” amesistiza RC Chalamila.

Mwisho askofu wa kanisa hilo Stella mate amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kushiriki nao katika kongamano hilo ambapo amemuomba kupeleka Salamu za shukrani kwa Rais pamoja zawadi ya tuzo na vitabu kwa ajili ya Rais Dkt Samia Suluhu lakini pia RC Chalamila amepatiwa tuzo na vitabu.