Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila leo Machi 01,2024 akiongea na vyombo vya habari Ofisini kwake Ilala Boma amewaomba wananchi hususani wakazi wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi katika barabara ambazo mwili huo utapita na uwanjani ambako mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi utaagwa rasmi.

RC Chalamila ametaja njia ambayo mwili wa Hayati utapitishwa ukitokea Mikocheni, utapelekwa Kinondoni Bakwata kwa ajili ya Dua ambayo itaongonzwa Shekh Mkuu wa Tanzania Dkt Abubakar Zuber, ukiwa inaelekea uwanja wa Uhuru, utapita Kinondoni- Kigogo- Ilala Boma-Veta-DUCE hadi Uwanja wa Uhuru-Temeke

Aidha RC Chalamila amesema kuanzia Saa 2:00 Asubuhi uwanja wa Uhuru uko wazi wananchi waingie ili kuaga mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi Rais wa awamu ya pili.

Pia RC Chalamila ametangaza kusitisha kwa shughuli za Serikali katika Mkoa ili watumishi, wanafunzi na makundi mengine waweze kushiriki kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya pili katika uwanja wa Uhuru

Sambamba na hilo RC Chalamila amesema Mkoa uko Shwari Usalama uko imara vyombo vyote vya usalama viko imara ” maombolezo ni siku 7 kama Mhe Rais Dkt Samia alivyotangaza tuendelee kumuombea Mzee wetu Hayati Ali Hassan Mwinyi” Alisema RC Chalamila

Mwisho: Hakika Sisi Wote ni Wa Mwenyezi Mungu, na Kwake Tutarejea.