Waziri Silaa abomoa ghorofa Mbezi Beach

Na Isri Mohamed


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amesimamia zoezi la ubomoaji wa ghorofa moja lililopo kwenye eneo la kiwanja no. 424 Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.


Waziri Silaa amesimamia zoezi hilo kwa lengo la kurudisha eneo hilo kwa mmiliki wake anayefahamika kwa jina la Naomi, baada ya kuhangaika kwa zaidi ya miaka 20 kurudisha eneo lake kutoka mikononi mwa bwana Maululu aliyekuwa akilimiliki kimakosa.

Kufuatia zoezi hilo Waziri Silaa ametoa onyo kwa mwananchi yeyote nchini aliyejenga au kumiliki eneo ambalo sio lake aondoke haraka kabla mkono wa sharia haujamfikia.