Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amemuelekeza Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu kushughulikia maadili ya kitabibu kwa madaktari wanaokiuka taratibu za kitabibu na kutoa taarifa za faragha za wagonjwa hadharani.

Ummy ametoa maelekezo hayo kufuatia taarifa iliyotolewa na Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sokoine Lindi, Dk Baraka Steven kuzungumzia faragha ya mgonjwa kinyume na maadili ya kitabibu ambayo inaelekeza taarifa za mgonjwa ni siri.

Kufuatia taarifa iliyotolewa na mtandao wa EATV, wadau mbalimbali waliibuka na kujadili iwapo ni sahihi kwa daktari kuzungumza na vyombo vya habari kuelezea faragha za mgonjwa bila ridhaa yake.

“Faragha ya mgonjwa ni moja kati ya sheria kuu chache za taaluma ya afya, hapa tuna taarifa zote za mgonjwa kuanzia jina, umri, jinsi yake, makazi na ugonjwa wake, tumeweka taarifa zake za siri kuwa taairfa ya habari” alihoji Sales Nicco.

“Upo sawa, hii ni kinyume na ethics za kitabibu. Namuelekeza Mganga Mkuu wa Serikali kulifuatilia na kunipatia Taarifa” amesema Ummy akimjibu Nicco.

By Jamhuri