Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Wasafi, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platinumz’ kufuatia kifo cha baba yake aliyekuwa Rais wa awamu ya pili hayati Ali Hassan Mwinyi.

Aidha, Rais Dk Mwinyi ameushukuru uongozi wa Wasafi kwa kuja kumfariji na kushiriki katika mazishi ya kiongozi huyo pamoja na utayari wao kushiriki kutangaza mazuri yanayofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Diamond amempongeza Rais Dk Mwinyi kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuwaletea maendeleo Wazanzibari na kuvuka malengo ya ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 hususani katika sekta ya elimu.

Wasafi wameahidi kuendelea kushirikiana na Rais Dk Mwinyi na kumuunga mkono kuyatangaza mazuri yote anayotekeleza kwa wananchi wa Zanzibar, pia wamemkabidhi zawadi ya nyimbo maalum kwa ajili ya kazi nzuri alizofanya iliyotungwa na wasanii kutoka Wasafi.

By Jamhuri