Na Mwandishi Wetu,Tarime

Halmashauri ya Tarime Vijijini imepokea jumla ya shilingi Bilioni 7.374,230,582 kwa ajili ya utakelezaji wa miradi mbalimbali ya jamii katika vijijini vilivyopo ndani ya Halmashauri hiyo.

Pesa za CSR ni pesa za utekelezaji huduma kwa jamii zinazotolewa na Mgodi wa Barrick kwa ajili ya miradi ya Jamii ambapo Halmashauri husimamia utekelezaji kwa maeneo husika.

Akizingumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Solomon Shati alisema pesa hizo zimetolewa kutekeleza miradi kwa miaka miwili mfururizo.

Alisema pesa hizo hutolewa kulingana na uzalisaji wa Mgodi na miradi hupitia mchakato kuanzia ngazi ya WDC,CMT hadi Wizara ya fedha ikipitishiwa mgodi hutoa pesa na Halmashauri inasimamia miradi inatekelewa.

“Mchakato unaanzia Vijijini wanaangalia vipaumbele vyao wanahitaji kitu gani uongozi wa Kijiji wanakaa kikao cha WDC wanajadili wanakuja tunakaa kikao na watu wa Mgodi tunajadili mradi unachakatwa na watalamu ukikubaliwa tunatuma Wizara ya fedha ” alisema.

Alisema hakuna mradi unatelezwa bila kupitia Wizara ya fedha na kuongeza kuwa zamani pesa za CSR zilikuwa zikitolewa na Watu wa Mgodi bila kufika eneo la mradi lakini kwa sasa wanafika na kijirishisha Wizara ikipitisha wanatoa pesa.

Alifafanua juu ya mugawayo wa fedha hizo kuwa baadhi ya Vijiji 11 vinavyozunguka Mgodi kati ya Kata 21 vinapata asilimia 70 ya pesa hizo na Vijiji vilivyo nje vinapata asilimia 30 ya pesa hiyo.

Vijiji vinavyopata asilimia 70 ni Matongo,Mjini kati,Nyagoto,Kewanja, Nyabichune,Kerende,Nyakunguru,Komarera, Nyamwaga,Msege pamoja na Genkuru.

Hata hivyo pesa hizo zinatekeleza miradi kiuchumi kwenye elimu kwa kujenga mashule,nyumba za walimu, kutengeneza madawati vile vile zinatumika kujenga vituo vya afya na zahanati pamoja na miradi inayoibuliwa .

Akiendelea kuzungumza alisema kuwa miradi lazima iwe kwenye kiwango cha fedha kuanzia bilioni 4 zinazalishwa kwa mwaka na mgodi ingawa inategemea na uzalishaji kwani Mgodi hukaa kikao na Halmashauri na kuwajulisha pesa iliyozaliswa .

Hata hivyo amesema bilioni 7 uliyotolewa kwa miaka miwili ni kulingana na kanuni ambapo pesa inatolewa kulingana na uzalishaji uliopatikana kwa mwaka na kuongeza kuwa katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka miradi mbali mbali imetekelezwa.

Miradi mikubwa ambayo imetekelezwa ni pamoja na mradi wa maji Kata ya Matongo ambao umeghalimu shilingi Milioni 998,946,584 , kituo cha afya kiiji cha Genkuru shilingi Milioni 151 mradi wa jengo la RCH Mama na Mtoto kikiji cha Msege Milioni 100 jengo liko kwenye hatua ya mwisho.

Aidha miradi hiyo ni mingi mikubwa na midogo ila kwa uchache ni kama vile ujenzi wa wood ya Watoto kituo cha afya Nyamongo pamoja na ununzi wa vifaa tiba jumla Milioni 53 ,nyumba ya mtumishi wa afya Kijiji cha Komarera shilingi milioni 70 .

Vilevile Halmashauri hiyo kwa kupitia pesa za mapato ya ndani imetumia Milioni 500 kutekeleza miradi mbali mbali kama vile kujenga kituo cha afya Kijiji cha kwihancha kujenga jengo la wagonjwa wa nje OPD,Mama na Mtoto,maabara pamoja na jengo la kufulia nguo pamoja na zahanati ya Komaswa iliyogharimu Milioni 83 pesa za ndani Milioni 33 na kutoka Serikali kuu Milioni 50.

By Jamhuri