Na Helena Magabe, JamhuriMedia, Tarime

Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 yanaonyesha kuwa ,idadi ya watu chini imeongezeka kutoka milioni 44,928,923 watu waliohesabiwa mwaka 2012 hadi kufikia watu milioni 61,741,120 kwa mwaka 2022 sawa na wastani wa ongezeko la idadi ya watu kwa mwaka la asilimia 3.2 kwa Tanzania Bara kwa upande wa Zanzibar idadi ya watu imeongezeka kutoka watu milioni 43,625,354 kutoka mwaka 2012 na kufikia kufikia watu milioni 1,889,773 mwaka 2022 sawa na wastani 1.9 hivyo kuanzia 2012-2022 kuna ongezeko la watu milioni 16.812,197 katika kipindi cha miaka 10.

Matokeo ya Sensa ya mwaka 2022 yamebainisha kuwa wanaume Tanzania bara ni milioni 29.1 na wanawake ni milioni 30.7 kwa upande wa Zanzibar wanaume ni milioni 0.9 na wanawake ni 1.0 jinsia ya kiume kwa upande wa Tanzania bara pamoja na Tanzania Zanzibar ni asilimia 49 huku wanawake wakiwa na asilimia 51 hata hivyo idadi ya watu inakadiliwa kuongezeka mara mbili baada ya miaka 22 itakapofika mwaka 2044.

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ina mikoa 31 ambapo mikoa 26 iko Tanzania Bara na mikoa mitano 5 iko Zanzibar matokeo ya 2022 yanaonyesha mikoa inayoongoza kuwa na idadi ya watu wengi ni Dar es Salaam ikiwa na watu milioni 5,383,728,sawa na asilimia 8.7 ya watu wote nchini, mkoa unaofatia ni Mwanza wenye watu milioni 3,699.872,Tabora watu milioni 3,391,679, Morogoro watu milioni 3,197,104 pamoja na Dodoma watu milioni 3,085,625 huku Mkoa wa Njombe ukiwa na idadi ndogo ya watu nchini ambao ni laki 889,946

Sensa ya Watu na Makazi maana yake ni utaratibu wa kukusanya, kuchukua, kuchambua, kutathimini, kuchapisha kusambaza pamoja na kutunza takwimu za kidemografia ,kiuchumi pamoja na mazingira wanayoishi katika nchi kwa kipindi maalumu ambapo utaratibu huo huwezesha kupatikana kwa taarifa za msingi za takwimu kama idadi ya Watu wote kwenye nchi kwa umri, jinsia,hali ya ulemavu,hali ya elimu,shughuli za kiuchumi,hali ya makazi na uzazi,vifo na ninginezo.

Kila baada ya miaka kumi Watanzania wanafanyiwa sensa kwa kuhesabiwa ikiwa ni kwa mujibu wa sharia ya takwimu sura no. 351 ambayo inailekeza Serikali kufanya sensa ya watu na makazi hata hivyo sensa hufanyika kukidhi matakwa ya Umoja wa Mataifa unaozitaka nchi kufanya sensa angalau mara moja kila baada ya miaka kumi hata hivyo lengo ni kupata viashiria vya msingi vya watu na makazi ambavyo vitawezesha katika kutunga sera,kupanga,na kufatilia mipango ya maendeleo ya kimkakati.

Sensa ya Watu na makazi ya mwaka 2022 imefanyika katika kipindi cha utekelezaji wa mpango mkakati wa umoja wa Mataifa wa kufanya sensa katika miaka 2020 ambao ulianzia 2015 na utaishia 2024 sensa ilianza kufanyika nchini Tanzania kwa mara ya kwanza mwaka 1967 na baada ya hapo mwaka 1978,1988,2002,2012 na mwaka jana 2022 matokeo ya sensa ya 2022 ni kwa ajili ya Mipango Jumuishi na Maendeleo Endelevu ya Nchi kwenye ugawaji rasimali zilizopo kulinana na uwiano wa watu katika ngazi zote za utawala.

Sensa hii ya mwaka 2022 chini ya usimamizi wa Ofisi ya takwimu ya Taifa(NBS) National Bereau stastistics imekuwa ya kitofauti kufuatia kufanyika kiteknolojia tofauti na zilizofanyika miaka ya nyuma hii ilitutumia teknolojia ya kidijitali katika utekelezaji wake kuanzia kwenye zoezi la utengaji wa maeneo ya kijografia ya kuhesabu watu kuanzia ngazi ya sheria,mitaa na vitogoji hadi kwenye zoezi la kuhesabu watu kwa kutumia vishikwambi(tables)katika hatua zote za utekelezaji wa zoezi hilo.

Kwanini sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 iwe ya kipekee na yakufanikiwa kuliko vipindi vingine vilivyopita hii ni kwa sababu iliongezeka sensa ya majengo na anwani za makazi ikiwa ni kwa mara ya kwanza sensa hii kufanyika tangu kuasisiwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 ingawa taarifa za majengo zilikuwa zikikusanywa katika tafiti za Kitaifa kila baada ya miaka mitano kwa ajili ya kudumisha sera ya mipango nchi.

Hata hivyo zoezi hili la uwekaji wa anwani za makazi ni endelevu hivyo basi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zitaendelea na zoezi hilo la uwekaji anwani za makazi pamoja na ukusanyaji wa taarifa za majengo yote yanayotarajiwa kujengwa nchini ili kuweza kuhusika kazi data za mjengo na anwani za makazi.


Sensa ya Watu na makazi ya mwaka 2022 imekusanya taarifa nyingi zaidi kwa sababu usomaji wa majira nukta katika kaya, majengo,ukusanyaji wa taarifa katika huduma zote za jamii vishikwambi vilitumika na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa kuboroshwa taarifa zilizokusanywa ukulinganisha na mwaka 2012 kwani dodoso kuu la maswali la mwaka 2022 lilikuwa na masala 100 ambapo dodoso kuu la mwaka 2012 lilikuwa na maswali 64.

Utekelezaji huu wa sensa ya majengo na anwani za makazi kwa kutumia mfumo wa teknolojia ulifanyika kwa lengo la kuongeza ufanisi na kupunguzia Serikali gharama ya kufanya mazoezi matatu makubwa katika vipindi tofauti ambapo taarifa za majengo na anwani za makazi ni kielelezo muhimu sana kwa Taifa na kwa Mwananchi mmoja mmoja kwa ajiri ya makazi na shughuli nyingine muhimu za kimaendeleo .

Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ilitimiza wajibu wake wa kufanya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kama zilivyokuwa zikifanyika kila baada ya miaka kumi hali kadhalika kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi naye alitimiza wajibu wake wakufanya Sensa ya Watu na Makazi.

Hata hivyo Rais Samia Suluhu Hassan alifanikisha zoezi hilo kwa kushirikiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Isdor Mpango, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi, Kassim Majaliwa Majaliwa(Mb) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Sensa ya Watu na makazi ya mwaka 2022.

Wengine ni Othman Masoud Othman Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar ,Hemed Suleiman Abdulla (MBW) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 , Spika Mstaafu wa Bunge Anne Semamba Makinda ambaye alikuwa Kamisaa wa sBensa Tanzania bara pamoja na Balozi Mohamed Haji Hamza ambaye alikuwa Kamisaa wa Sensa Zanzibar.

Kwa upande wa Zanzibar Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi alifanikiwa zoezi la sensa 2022 kwa kupitia Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa(Mb),Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla,(MBW) wajumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa, Kamati ya Taifa ya Ushauri ya Sensa,Kamati ya Ushauri ya kiufundi,Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar,wakuu wa mikoa,wakuu wa wilaya,madiwani,Wwratibu wa sensa Taifa,waratibu wa sensa wa mikoa na wilaya,viongozi wa Kata,Mitaa na Vitongoji,wasimamizi makarani wa sensa Wakuu wa Kaya pamoja na vyombo ya habari.

Spika mstafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Anne Semamba Makinda Kamisaa wa Sensa Tanzania Bara , Balozi Mohamed Haji Hamza Kamisaa wa sensa Zanzibar,Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu Zanzibar, Dkt Amina Msengwa, Mwenyekiti wa bodi ya Takwimu Zanzibar, Balozi Amina Salum Ali,Ofisi ya Takwimu Taifa (NBS) chini ya uongozi wa Dk Albina Chuwa,Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar (OCGS) Bw.Salum Kasim Ali, watumishi wa idara ya ardhi nyumba maendeleo na makazi,Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia na Habari pamoja na Watumishi wengine wa Serikali.

Hata hivyo yapo Mashirika yaliyofadhili zoezi la sensa 2022 UNFPA, UN Womas, UNICEF, USAID, IOM, FCDO, Benki ya Dunia,Ofisi ya Sensa ya Marekan i(US Census Bureau), Ubalozi wa Korea kusini nchini Tanzania pamoja na washirika wengine wa maendeleo.

By Jamhuri