Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhesshimiwa Innocent Bashungwa amesema kuwa, katika kipindi cha mwezi Julai hadi Juni 2022 halmashauri nchini zimekusanya Shilingi Bilioni 888.7 ambayo ni asilimia 103 ya makisio ya mwaka husika.

Ameyasema hayo leo Agosti 2,2022 jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu mapato na matumizi ya ndani ya halmashauri kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

HALI YA MAKUSANYO YA HALMASHAURI KWA KIPINDI CHA MIAKA 10 MFULULIZO KUANZIA MWAKA 2012-2013 HADI MWAKA 2021/2022

Bashungwa amesema kuwa, katika mwaka wa fedha 2021/22, halmashauri zilipanga kukusanya Shilingi Bilioni 863.9 kutoka kwenye vyanzo vya mapato ya ndani.

“Katika kipindi cha mwezi Julai hadi Juni 2022, Halmashauri zimekusanya Shilingi Bilioni 888.7 ambayo ni asilimia 103 ya makisio ya mwaka husika.

“Uchambuzi wa taarifa za mapato ya ndani ya halmashauri katika mwaka wa fedha 2021/22, unaonesha kuwepo kwa ongezeko la mapato halisi yaliyokusanywa kwa kiasi cha Shilingi bilioni 131.7, ikilinganishwa na kiasi halisi kilichokusanywa katika mwaka wa fedha 2020/21, cha Shilingi Bilioni 757.1, sawa na ongezeko la asilimia 17,”amesema Mheshimiwa Bashungwa.

Amesema, kiwango hicho hakijawahi kufikiwa kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita, kwani Halmashauri hazijawahi kufikia malengo yao ya mwaka kwa asilimia 100.

By Jamhuri