Dar es Salaam
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, amesema Serikali imetenga Shilingi trilioni 2.46, sawa na asilimia 97.5 ya bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2026/27, kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta ya nishati.
Amesema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuhakikisha nchi inakuwa na nishati ya uhakika, ya kutosha na inayokidhi mahitaji ya wananchi pamoja na shughuli za kiuchumi.
Mhe. Homera amesema Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaendelea kuweka msukumo katika kukuza sekta ya nishati ili iwe kichocheo cha ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi.
Ametoa kauli hiyo leo, Oktoba 7, 2026, wakati akifungua Maonesho ya 10 ya Kimataifa ya Biashara ya Nishati ya Umeme na Nishati ya Jua (Power and Solar Energy International Trade Event), yanayofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Expo Centre, jijini Dar es Salaam, kuanzia Oktoba 7 hadi 10, 2026.
Amesema kupitia bajeti hiyo, Serikali itaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwemo Mradi wa Kufua Umeme kwa Maji wa Julius Nyerere pamoja na Mradi wa Umeme wa Jua wa Kishapu, ambapo megawati 50 tayari zimeunganishwa kwenye Gridi ya Taifa na awamu ya pili inatarajiwa kuongeza megawati 100.
Kwa mujibu wa Mhe. Homera, bajeti hiyo pia inalenga kuharakisha utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kitaifa, ikiwemo Ajenda ya Mission 300 inayolenga kuunganisha wateja wapya wa umeme milioni 1.7 kila mwaka na kufikisha jumla ya wateja milioni 8.3 ifikapo mwaka 2030.
Aidha, amesema Serikali inaendelea kutekeleza Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia wa mwaka 2024–2034, wenye lengo la kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.
Ametaja pia Mradi wa Umeme Vijijini kupitia mpango wa kupeleka umeme katika vitongoji 9,009 ifikapo mwaka 2030, kwa gharama ya Shilingi trilioni 1.2, pamoja na kuimarisha mchanganyiko wa vyanzo vya nishati (Energy Mix) kwa kuongeza mchango wa nishati jadidifu kutoka asilimia 61.8 hadi asilimia 75 ifikapo mwaka 2030.
Waziri Homera amesisitiza kuwa utekelezaji wa miradi hiyo unahitaji ushiriki mkubwa wa sekta binafsi, hususan wawekezaji na wadau wenye teknolojia, mitaji na ujuzi wa kisasa, ili kuongeza kasi ya maendeleo ya sekta ya nishati na kuendana na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Maonesho hayo yamewakutanisha wawekezaji, wazalishaji na wasambazaji wa teknolojia za nishati ya umeme na nishati ya jua kutoka nchi 48 duniani, kwa lengo la kuonesha teknolojia na suluhisho mbalimbali zinazoweza kuchangia katika maendeleo ya sekta ya nishati.
Mhe. Homera amewahimiza Watanzania kutembelea mabanda mbalimbali katika maonesho hayo ili kujionea teknolojia zinazotumika katika sekta ya nishati, kujifunza na kuongeza uelewa kuhusu fursa na ubunifu unaoendelea katika sekta hiyo.‘TRILIONI 2.46 ZATENGWA KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO YA NISHATI’ MHE. HOMERA
Dar es Salaam
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, amesema Serikali imetenga Shilingi trilioni 2.46, sawa na asilimia 97.5 ya bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2026/27, kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta ya nishati.
Amesema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuhakikisha nchi inakuwa na nishati ya uhakika, ya kutosha na inayokidhi mahitaji ya wananchi pamoja na shughuli za kiuchumi.
Mhe. Homera amesema Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaendelea kuweka msukumo katika kukuza sekta ya nishati ili iwe kichocheo cha ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi.
Ametoa kauli hiyo leo, Oktoba 7, 2026, wakati akifungua Maonesho ya 10 ya Kimataifa ya Biashara ya Nishati ya Umeme na Nishati ya Jua (Power and Solar Energy International Trade Event), yanayofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Expo Centre, jijini Dar es Salaam, kuanzia Oktoba 7 hadi 10, 2026.
Amesema kupitia bajeti hiyo, Serikali itaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwemo Mradi wa Kufua Umeme kwa Maji wa Julius Nyerere pamoja na Mradi wa Umeme wa Jua wa Kishapu, ambapo megawati 50 tayari zimeunganishwa kwenye Gridi ya Taifa na awamu ya pili inatarajiwa kuongeza megawati 100.
Kwa mujibu wa Mhe. Homera, bajeti hiyo pia inalenga kuharakisha utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kitaifa, ikiwemo Ajenda ya Mission 300 inayolenga kuunganisha wateja wapya wa umeme milioni 1.7 kila mwaka na kufikisha jumla ya wateja milioni 8.3 ifikapo mwaka 2030.
Aidha, amesema Serikali inaendelea kutekeleza Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia wa mwaka 2024–2034, wenye lengo la kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.
Ametaja pia Mradi wa Umeme Vijijini kupitia mpango wa kupeleka umeme katika vitongoji 9,009 ifikapo mwaka 2030, kwa gharama ya Shilingi trilioni 1.2, pamoja na kuimarisha mchanganyiko wa vyanzo vya nishati (Energy Mix) kwa kuongeza mchango wa nishati jadidifu kutoka asilimia 61.8 hadi asilimia 75 ifikapo mwaka 2030.
Waziri Homera amesisitiza kuwa utekelezaji wa miradi hiyo unahitaji ushiriki mkubwa wa sekta binafsi, hususan wawekezaji na wadau wenye teknolojia, mitaji na ujuzi wa kisasa, ili kuongeza kasi ya maendeleo ya sekta ya nishati na kuendana na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Maonesho hayo yamewakutanisha wawekezaji, wazalishaji na wasambazaji wa teknolojia za nishati ya umeme na nishati ya jua kutoka nchi 48 duniani, kwa lengo la kuonesha teknolojia na suluhisho mbalimbali zinazoweza kuchangia katika maendeleo ya sekta ya nishati.
Mhe‘TRILIONI 2.46 ZATENGWA KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO YA NISHATI’ MHE. HOMERA

Mhe. Homera amewahimiza Watanzania kutembelea mabanda mbalimbali katika maonesho hayo ili kujionea teknolojia zinazotumika katika sekta ya nishati, kujifunza na kuongeza uelewa kuhusu fursa na ubunifu unaoendelea katika sekta hiyo.Homera amewahimiza Watanzania kutembelea mabanda mbalimbali katika maonesho hayo ili kujionea teknolojia zinazotumika katika sekta ya nishati, kujifunza na kuongeza uelewa kuhusu fursa na ubunifu unaoendelea katika sekta hiyo.