Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Camillus Wambura, amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Matride Kuyeto kutoka Kamanda wa Polisi Kikosi cha Reli kwenda kuwa Kamanda wa Polisi (RPC) Mkoa wa Singida.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa Jeshi la Polisi kwa vyombo vya habari, imesema Kamanda Matride Kuyeto anakwenda kuchukuwa nafasi ya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Amon Kakwale ambaye amestaafu utumishi wa Umma kwa mujibu wa sheria.


