Jumuiya ya Kimataifa na Amani imemtangaza Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mshindi wa tuzo mbili za kimataifa ikiwemo ya amani duniani 2022.

Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Gaudencia Kabaka, amesema Rais Samia ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo hizo wiki iliyopita na atakabidhiwa tuzo hiyo Oktoba 24, mwaka huu.

Amesema hayo leo Oktoba Mosi, 2022 kuwa mambo yaliyomfanya Rais Samia kupata tuzo hizo ni uboreshaji wa miundombinu ya afya na elimu ndani ya kipindi kifupi cha uongozi, utetezi wa masuala ya amani ikiwemo uhuru wa kuabudu na amani.

Mengine ni kujali masuala ya kijinsia kwa kuteua wanawake wengi katika uongozi, ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari na msingi na utoaji wa elimu bila malipo.

Tuzo nyingine aliyotangazwa kuwa mshindi ni Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika kuipata ni tuzo ya Rais wa Dhahabu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Maraisi waliowahi kupata tuzo kwa Afrika hizo ni Rais wa Liberia, George Weah na Rais wa Botswana Ian Tseretse Khama.Rais Samia atakabidhiwa Oktoba 24, mwaka huu.

By Jamhuri