Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Kamati ya siasa ya Mkoa wa Dar es Salaam leo Novemba 30, 2023 imefanya ziara ya kukagua barabara zinazojengwa na kusimamiwa na TANROADS ikiwemo hiyo inayotoka Kibamba shule kuelekea Mpiji Magohe yenye urefu wa KM 9.2  kwa gharama ya bilioni 2.7 kwa kiwango cha lami.

Wakiongozwa na Katibu wa CCM Mkoa wa DSM Mh. Adam Ngalawa alisema barabara hiyo inajengwa kwa fedha za mapato ya ndani kwa usimamizi wa TANROADS na kamati imeridhishwa na hatua waliyofikia, mpaka sasa KM 2 zimeshakamilika na ujenzi unaoendelea ni KM 1.5  unaotarajia kukamilika Mei 2024.

“Niwaombe wananchi wa Dar es salaam waendelee kumwamini Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya na chini ya wataalamu wetu kazi inaendelea.” Alisema Mhe. Ngalawa.

Naye Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa akitokea Dar es salaam Juma S. Gaddafi alipongeza ujenzi huo unaoendelea ambapo kumeongeza ujenzi wa nyumba za kuishi za kisasa kutokana na uwepo wa barabara zinazorahisisha usafiri wa wakazi wa maeneo hayo.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kibamba Sembuli M. Mgendi alitoa shukrani kwa Mhe Rais Dkt Samia kwa utekelezaji wa Ilani kutafuta fedha nyingi za miradi mikubwa inayoenda kwa wakati na aliahidi wataitunza miundombinu ili salama. 

Awali kamati hiyo ilitembelea na kukagua ujenzi wa barabara ya mwendokasi itokayo mjini kwenda Gongo la Mboto (BRT3), hawakuridhishwa na hatua waliyofikia na kutaka kasi ya usimamizi iongezeke ambapo mradi huo mpaka sasa umekamilika kwa asiliamia 23 ambao ulianza tangu Agusti 2022 na unatakiwa ukamilike wote April 2024.

By Jamhuri