Na Mussa Augustine,JamhuriMedia

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokratic Party (DP), Abdul Mluya amemuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuunda Wizara Mpya ya Umwagiliaji ambayo itajikita katika kuhakikisha inajibu hoja za sekta ya umwagiliaji.

Hayo ameyasema Dar es Salaam Januari 13,2023 wakati akizungumza na JAMHURI DIGITAL kuhusu masuala mbalimbali ambapo amebainisha kuwa endapo Serikali itaanzisha Wizara ya Umwagiliaji itashirikiana na Wizara ya Kilimo pamoja na Wizara ya Maliasili nakusaidia kutunza Mazingira na Kuondokana na Changamoto za Mabadiliko ya Tabiachi ambayo yanasababisha hali ya Ukame nchini.

Katibu mkuu huyo wa DP amesema kwamba Sekta ya Umwagiliaji ikiimalishwa itasaidia kuondokana na kilimo cha kutegemea mvua za masika na vuli hii ni kutokana na kuwepo kwa uoto wa asili ambao utatunza mazingira nakuweza kupata maji ya kutosha kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.

“Katika nchi ambazo Mungu aliumba duniani nchi ya Tanganyika aliiumba kwa mfano wake Tanganyika ina mito mingi,ina maziwa na mabonde tunaweza kufanya kilimo cha umwagiliaji bila hata tatizo ni suala la utaalamu tu ambapo anatakiwa kuwepo waziri mwenye dhamana ya Umwagiliaji ambaye atajibu hoja za sekta hiyo Bungeni.” amesema Mluya.

Nakuongeza Kwamba “Sekta ya umwagiliaji ikisimamiwa ipasavyo Tanzania ina uwezo mkubwa wa kuzalisha chakula kwa wingi na kuweza kuziuzia nchi Jjrani ambazo zinakumbwa na uhaba wa chakula.

Akizungmzia kuhusu masuala ya kisiasa Mluya amesema kwamba miaka sita iliyopita hali ya siasa ilidhoofika kutokana na vyama vya siasa kuzuiliwa kufanya mikutano ya hadhara hali ambayo ilikuwa ni ukandamizwaji wa haki kikatiba.

Aidha amesema kuwa kufuatia Rais Dkt.Samia kuruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, itasaidia vyama hivyo kunadi sera zake kwa wananchi na kuwafanya wawe huru kuchagua kiongozi wanayemtaka kwa ajili ya kuwaletea maendeleo.

“Cha msingi sisi wanasiasa tujue tulikosea wapi na tujirekebishe,tujue wananchi wanataka nini,tuna wajibu wa kunadi sera zetu kuikosoa serikali iliyopo madarakani bila kuvunja amani ya Taifa letu na Wananchi kwa ujumla”amesema Mluya.

Hata hiyvyo Mluya amesema kuwa Jeshi la Polisi linapaswa kuvilinda vyama vya siasa kwa mujibu wa Katiba,hivyo amelisihi Jeshi la Polisi lisiwe sehemu ya chanzo cha Vurugu badala yake litoe vibali kwa wakati na pia kuhakikisha usalama wa Wananchi na Viongozi wa Vyama vya siasa unatekelezwa katika maeneo ambayo vyama vya siasa vinafanya shughuli zake.

Amesema kuwa Chama Cha Demokratic Party (DP) kimeanza kufanya mikutano yake ya ndani ikiwa ni sehemu ya programu ambayo ilipanga kufanya kabla ya kutolewa kwa tangazo la kuruhusu vyama vya Siasa kufanya mikutano yake ya hadhara nakwamba baada ya programu hiyo chama hicho kitaanza kufanya mikutano ya hadhara ili kunadi sera zake kwa wananchi.

By Jamhuri