Na Theophilida Felician, JamhuriMedia Dodoma.
Chama cha Waganga wa Tiba Asili (TAMESOT) kimesikitishwa na tukio la mauaji ya kikatili yakimuhusisha mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM James Rojas Temba aliyeuawa kwa kutenganishwa kichwa na kiwiliwili hivi karibuni mkoani Dar es salaam.
Kauli hiyo imetolewa naye Katibu Mkuu wa TAMESOT, Lukasi Joseph Mlipu akiwa kwenye tukio la kuwahamasisha waganga kushiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo na weledi yanayotarajia kufanyika Juni mwaka huu wa 2026 yanayoandaliwa na chama hicho kwa kushirikiana na chuo cha sayansi shirikishi DIHAS Milembe Dodoma, Wizara ya Afya, TAMISEMI na Maliasili.
Kiongozi huyo ambaye amekutana na waganga makao makuu ya ofisi za chama hicho Kibaigwa mkoani Dodoma amesema wameguswa na tukio hilo ambalo nila ukatili wa hali ya juu.
Amefafanua kwamba kauli ya TAMESOT imekuja baada ya kutolewa ripoti ya Jeshi la Polisi ikielezea kuwashikilia watu kadhaa wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo akiwemo mmoja wao Said Ally ayelitambulika kuwa mganga wa tiba asili.
Amesema matukio ya yanamna hiyo niya kulaniwa kwa nguvu zote, ambapo ameviomba vyombo vya dola kufanya uchunguzi kwa kina na watakaobainika kuhusika na tukio la mwanafunzi Temba wachukuliwe hatua kali kwa mjibu wa sheria huku akitoa pole kwa familia, ndugu jamaa na watanzania wote kwa msiba wa James Temba.
Pia amesisitiza kuwa tiba asili ni huduma muhimu kwa jamii tangu na tangu hivyo hapaswi mtu yeyote kuibeza au kuichafua kwakutumia jina la mwavuli wa taaluma hiyo ili kusababisha madhara yakikatali kwa wananchi na TAMESOT itaendelea kuunga mkono juhudi za serikali kuwahimiza waganga kufanya kazi kwa kufuata kanuni na taratibu husika ikiwemo usajili.
Aidha ameongeza kuwa mtu anayebainika kuhusika na vitendo viovu simganga halisi bali ni mhalifu kama wahalifu wengine hivyo ya paswa wachukuliwe hatua ipasavyo.
Hata hivyo ameyataja mapendekezo ya TAMESOT katika kukabiliana na hayo ni pamoja na kutoa elimu kwa waganga na jamii kwa ujumla ili kuuzuia uhalifu usiendelee kutokea na waganga wote kusajiliwa.
Amehitimisha akiiomba serikali kuwapatia ushirikiano TAMESOT katika mafunzo mbalimbali wanayotoa kwa waganga kutokana na chama hicho kuweka utaratibu juu ya kuwasaidia mafunzo yenye kuwajengea uwezo na weledi katika majukumu yao ya utoaji huduma ya tiba huku akiwasihi waganga kujiunga na vyama kikiwemo TAMESOT kwa manufaa zaidi.






