Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Katavi

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana amewasili mkoani Katavi kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi itakayokwenda sambambamba na kupokea taarifa na kukagua miradi ya maendeleo.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdulrahaman Kinana akisalimiana na viongozi wa Chama na Serikali mkoa wa Katavi baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mpanda kwa ajil ya kuanza ziara mkoani humo

Katika ziara hiyo ya kikazi ameongazana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Shaka Hamdu Shaka na baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege Katavi Kinana amepokelewa na Wana CCM Mkoa wa Katavi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Mkoa Beda Katani.

Baada ya kuwasili Kinana akiwa na Shaka wamepata nafasi ya kusalimiana na wanachama wa chama hicho na kisha kupokea taarifa ya CCM na Serikali Mkoa wa Katavi.

Akipokea taarifa hiyo Kinana ameelezwa hali ya mwenendo wa Chama na Serikali na kwa sehemu kubwa ameambiwa hali ni shwari na kwamba viongozi wamekuwa na ushirikiano mkubwa hali inayofanywa utekelezaji wa Ilani kufanyika kwa kiwango cha kuridhisha.

Kinana anatarajiwa kuzindua kituo cha afya,mradi wa fremu 15 za biashara, pia atatembelea mradi wa fremu za vibanda 188 pia atazungumza na WanaCCM na viongozi mbalimbali . Kinana atakuwa katika ziara ya mikoa ya Nyanda za Juu ukiwemo Mkoa wa Katavi na kisha kuelekea Mkoa Rukwa, Songwe na Mbeya.

By Jamhuri