Kuelekea Kombe la Dunia: Tembo Warriors wajifua kambini Uturuki

Timu ya Taifa ya Soka kwa Walemavu, Tembo Warriors imeendelea na maandalizi yao wakiwa kambi maalum nchini Uturuki waliyoandaliwa na Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kabla ya Oktoba Mosi kuanza mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia dhidi ya Hispania mjini Pendik.

Mazoezi hayo yameshuhudiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi ambaye amewasili nchini humo Septemba 27, 2022.

Mashindano hayo yanatarajiwa kufunguliwa kesho Septemba 30, 2022.