Fungu la fidia latengwa
Baada ya tathmini hiyo, Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ilitenga wastani wa Sh 8,050,000,000 kwa ajili ya kulipa fidia. Iliomba fedha hizi kutoka Hazina katika mchakato uliokuwa wa wazi kabisa.

Ilielezwa kuwa nyumba 233 zimeharibika kabisa (totally damaged), lakini ndani ya kundi hili kama inavyoonyesha sehemu ya orodha tuliyochapisha, baadhi ya watu walilipwa fidia ya hadi Sh 18,000, huku wengine wakiambulia hadi Sh milioni 60.

Fedha iliyotengwa kwa ajili ya kufidia nyumba hizo ni Sh 2,465,193,000. Hii ina maana kwa wastani kila nyumba ilipaswa kulipwa fidia ya Sh 1,058,022, lakini uchakachuaji ukaingia kati, ingawa kiasi hicho nacho bado kisingetosha kulingana na ukubwa wa uharibifu uliotokea.

Kundi la nyumba 54 zilizodaiwa kuwa zimeharibika kwa kiwango cha kutofaa tena, hawa walitengewa Sh milioni 906,486, ambazo kwa wastani ni sawa na Sh 16,785,837 kwa kila nyumba, lakini uhalisia wengine walilipwa zaidi.

Ukiacha nyumba hizo, kiasi cha Sh 4,627,156,250 kilitengwa kwa ajili ya kukarabati nyumba 9,031 zilizopata uharibifu mdogo wa hapa na pale. Kwa thamani za ndani, waathirika 186 walitengewa wastani wa Sh 51,242,000.

By Jamhuri