Marseille, Ufaransa

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel,
wamekutana mjini Marseille, Ufaransa
kujadiliana kuhusu uhamiaji haramu
kuelekea mkutano wa kilele wa Umoja wa
Ulaya Septemba 20, mwaka huu.
Akimkaribisha Merkel katika kasri ya Pharo
iliyoko katika mji wa Marseille, Macron
amesema watajadili changamoto
zinazohusu uhamiaji, kujitoa kwa nchi ya
Uingereza katika Jumuiya ya Ulaya na
mageuzi yanayohitajika kufanyika nchi za
Ulaya siku zijazo na mamlaka husika.
Katika kikao hicho kuhusu kujitoa kwa
Uingereza Jumuiya ya Ulaya, umeendelea
kuwa mjadala, ikiwa ni pamoja na kujadiliwa
na vyombo mbalimbali vya habari barani

Ulaya.
Uingereza inajiandaa kujiondoa katika
Umoja wa Ulaya ifikapo Machi 2019, ingawa
hadi sasa kuna machache tu yaliyowekwa
wazi kuhusu suala hilo.
Katika taarifa fupi ya pamoja baada ya kikao
hicho, Merkel amesema Ufaransa na
Ujerumani zinao mkakati wa pamoja
kuhusu namna ya kupambana na suala la
uhamiaji haramu unaoendelea kushika kasi
Afrika, Ulaya na sehemu zingine duniani.
Pia waliahidi kwa pamoja mpango wa
uendelezaji wa muungano wa sarafu, umoja
wa kibenki na kuimarisha kanda ya sarafu
ya euro na mada juu ya uhamiaji.
Pia walijadili uwezekano wa mipango
yenye ufanisi itakayoimarisha mipaka ya nje
ya Umoja wa Ulaya na kushauri kanda hiyo
kuonyesha mshikamano zaidi ili kupunguza
shinikizo la kiusalama kwa mataifa
wanakoingilia wahamiaji kama Ugiriki, Italia
na Hispania.
Viongozi hao walikubaliana kuhusu
mapendekezo ya kuanzisha bajeti ya kanda
ya euro kuanzia mwaka 2021 ndani ya
mfumo wa sasa wa kifedha, pamoja na

kanuni sawa za kibenki na mfumo wa
uokozi wa benki za ukopeshaji zinazofeli.
Macron na Merkel pia walijadili azima ya
Mbunge wa Ujerumani, Manfred Weber,
ambaye ni mwanachama wa muungano wa
vyama vya kihafidhina wa Markel ya
kuwania nafasi ya Rais wa Halmahsuri Kuu
ya Umoja wa Ulaya mwaka 2019.
Ingawa Merkel anaunga mkono ugombea
wa Weber, rais wa Ufaransa hakubaliani na
uamuzi wa kumuidhinisha mgombea kutoka
kambi ya vyama vya mrengo wa kati – kulia
wa European People’s Party (EPP), ambao
unahusisha pia chama cha Waziri Mkuu wa
Hungary, Viktor Orban, cha Fidesz.
Msemaji wa Merkel, Steffen Seibert,
amesema kabla ya kuondoka kwa kansela
huyo nchini Ufaransa, viongozi hao wawili
pia walizungumzia msimamo wa nchi zao
juu ya sera ya kigeni kuhusu Syria, Ukraine
na Balkan Magharibi.

Makala hii imeandikwa kwa msaada wa
mitandao.

Mwisho

Please follow and like us:
Pin Share