Magufuli Asaini Misamaha Ya Wafungwa

Rais John Magufuli amesaini nyaraka za wafungwa 63 ambapo wafungwa 61 walikuwa wamehukumiwa kunyongwa na wawili kifungo cha maisha. Nyaraka hizo alizisaini mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa huko Dodoma.
Katika msamaha huo wamo wanamuziki wawili, Nguza Viking na Papii Kocha waliokuwa wamehukumiwa kifungo cha maisha na ambao tayari waliachiwa jana.