Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Mama Regina Lowassa mke wa Waziri Mkuu Mstaafu (wa tatu kushoto) na Fredrick Lowassa (kulia) alipoenda kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Ngoyai Lowassa anayepata matibabu jijini Johannesburg, Afrika ya Kusini, Desemba 28, 2022. Wa pili kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa na kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa amemwakilisha Rais Dkt.Samia Hassan Sululu kumjulia hali Waziri Mkuu Mtsaafu Edward Ngoyai Lowassa anayeendelea na matibabu Afrika Kusini.

Akizungumza na wana familia kwa niaba ya Rais Samia, Waziri Mkuu amewasilisha salamu za pole kutoka kwa rais na kusema kuwa rais anafuatilia hali ya Lowasa kwa ukaribu na anamuombea afya njema.

Majaliwa ametoa salamu hizo leo Jumatano Desemba 28,2022 jijini jijini Johannesburg, Afrika ya Kusini ambako alikwenda kumjulia hali Lowasa.

Kwa upande wake mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,mama Regina Lowasa amemshukuru Rais kwa jinsi ambavyo amekuwa karibu na wana familia na ambavyo anafuatilia matibabu ya Lowasa.

Mtoto mkubwa wa Lowasa ambaye pia ni Mbunge Jimbo la Monduli Fredrick Lowassa amewashukuru Watanzania kwa maombi yao ya kumtakia afya njema baba yao.

By Jamhuri