Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipanda mti aina ya Mparachichi katika Skuli ya Sekondari Maziwang’ombe iliyopo Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati wa ufunguzi wa skuli hiyo ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka
60 ya Muungano.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akimwagilia mti aina ya Mparachichi mara baada ya kuupanda katika Skuli ya Sekondari Maziwang’ombe iliyopo Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati wa ufunguzi wa skuli hiyo ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akifurahi jambo akiwa na viongozi pamoja na wanafunzi wakati akikagua Skuli ya Sekondari Maziwang’ombe iliyopo Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati wa ufunguzi wa skuli hiyo ikiwa ni
Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akiwa ameketi pamoja na wanafunzi wa kidato cha kwanza wa Skuli ya Sekondari Maziwang’ombe iliyopo Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati wa ufunguzi wa skuli hiyo ikiwa ni Shamrashamra za Madhimisho ya Miaka 60 ya Muungano.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akisalimiana na Viongozi mbalimbali wakati akiwasili katika Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Maziwang’ombe iliyopo Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na Akram Juma ambaye ni wanafunzi wa kidato cha kwanza wa Skuli ya Sekondari Maziwang’ombe iliyopo Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati wa ufunguzi wa skuli hiyo ikiwa ni
Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali – Zanzibar Bw. Khamis Abdallah Said wakati akikagua Skuli ya Sekondari Maziwang’ombe iliyopo Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba katika ufunguzi wa skuli hiyo ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho
ya Miaka 60 ya Muungano.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akiweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Maziwang’ombe iliyopo Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akikata utepe kuashiria Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari
Maziwang’ombe iliyopo Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba ikiwa
ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano. Tarehe 21 Aprili
2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akihutubia viongozi na wananchi mbalimbali wakati wa Ufunguzi wa
Skuli ya Sekondari Maziwang’ombe iliyopo Wilaya ya Micheweni Mkoa wa
Kaskazini Pemba ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya
Muungano. Tarehe 21 Aprili 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akiwa katika picha ya pamoja na watoto mbalimbali wa Kijiji cha
Maziwang’ombe mara baada ya hafla ya Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari
Maziwang’ombe iliyopo Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba ikiwa
ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano. Tarehe 21 Aprili
2024.

                                                                              …………………..

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango ametoa wito kwa wazazi na walezi kusimamia kikamilifu elimu ya
watoto kwa kudhibiti utoro katika skuli pamoja na kuhakikisha watoto wa
kiume na wa kike wanaojiunga na skuli za msingi na sekondari wanamaliza
masomo.

Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati wa Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari
Maziwang’ombe iliyopo Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba ikiwa
ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano. Amesema ni
vema kuwaandikisha watoto wote wenye umri wa kwenda skuli, kuwafuatilia
maendeleo yao pamoja na kuwahimiza kusoma badala ya kushiriki katika
shughuli za uvuvi na nyinginezo. Amewasihi kutumia vema miundombinu
bora ya elimu iliyoandaliwa na serikali ili kuhakikisha watoto wanapata elimu
bora.

Aidha Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa jamii kushirikiana katika
malezi ya watoto kwa kufuata mila na desturi sahihi, maadili yaliyo mema na
kushika mafundisho ya dini ambayo yatawaepusha na maovu mengi katika
jamii inayowazunguka. Ametoa wito wa kuhakikisha hatua za kisheria
zinachukuliwa kwa watakaobainika kufanya unyanyasaji wa kijinsia na
kingono, kuoa au kusababisha mimba za utotoni ili kuzuia tabia ya watoto
kukatishwa masomo.

Makamu wa Rais ameongeza kwamba Serikali zote mbili zimedhamiria kuleta
usawa wa kijinsia kwa kuondosha mila na taratibu kandamizi. Ametaja tatizo
la ndoa za mapema Kaskazini Pemba linaathiri ustawi wa watoto wa kike na
hivyo kuwanyima fursa mbalimbali katika maisha.

Vilevile Makamu wa Rais amehimiza umuhimu wa kushirikiana katika kulinda
na kutunza mazingira. Amesema uchafuzi na uharibifu wa mazingira hapa
nchini kutokana na shughuli mbalimbali bado ni tatizo kubwa ambapo jitihada
kubwa za Serikali za maendeleo zinaathiriwa na changamoto hiyo.

Ametoa rai kwa Wakuu wa Skuli zote kuhakikisha kila mwanafunzi anaotesha
walau mti mmoja (matunda na kivuli) na kuutunza kwa kipindi chote
atakachokuwepo skuli. Aidha amewasihi wananchi kuotesha miti na kuitunza
katika makaazi yao na maeneo mengine.

Makamu wa Rais amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, zimejizatiti kuendelea kuulinda na
kuuimarisha Muungano kwa lengo la kudumisha amani, utulivu na kuwaletea
wananchi wote maendeleo. Amesema katika kipindi cha miaka 60 ya
Muungano mafanikio makubwa yamepatikana katika sekta ya elimu ikiwemo
Elimu kuwa ni haki ya msingi ya kila Mtanzania, Ongezeko la miundombinu ya
elimu, Ongezeko la vyuo na taasisi za Elimu ya Juu pamoja na Ongezeko la
Idadi ya wanafunzi kutoka Zanzibar wanaopata mikopo ya Elimu ya Juu
Amesema jitihada hizo za Serikali katika kuimarisha miundombinu ya elimu ni
endelevu na zinajumuisha upatikanaji wa vifaa mbalimbali vikiwemo vifaa vya
kufundishia na kujifunzia, samani na upatikanaji wa walimu wenye sifa.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali – Zanzibar Ali
Abdulgalam Hussein amesema ufunguzi wa skuli hiyo ni matunda ya
Muungano unaotimiza miaka 60. Amesema Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Amali itaendelea kutekeleza ilani ya uchaguzi kikamilifu ili kuhakikisha
malengo yaliowekwa yanafikiwa.

Ujenzi wa Skuli hiyo ya ghorofa tatu umegharimu shilingi bilioni 6.2. Shule
hiyo ni ya kwanza kwa upande wa sekondari katika kijiji cha Maziwang’ombe
ambapo ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 1850 kwa pamoja kwa wastani wa
wanafunzi 45 kila darasa.

By Jamhuri