Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Musoma Vijijini

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sosepter Muhongo kwa kushirikiana na viongozi wakiwemo wakuu wa Wilaya ya Musoma na Halmashauri yake (Musoma DC), waemeendesha harambee ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Etaro, ambayo itakuwa ya kata hiyo katika kisiwa cha Rukuba.

Katika tukio hilo lililofanyika Septemba 27, 2023 kwenye Kisiwa hicho,
Wafanyakazi wa kada mbalimbali, wakiwemo walimu, Kamati ya Siasa ya Wilaya na Wadau wengine wameshiriki.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Mbunge kupitia taarifa yake kwa umma, mapema leo Septemba 30,2023, imebainisha kuwa, michango iliyopatikana kwenye harambee hiyo ni pamoja na:

“Wakazi na wazaliwa wa Kisiwa cha Rukuba-Saruji Mifuko 167, Kamati ya Siasa ya Kata CCM-Saruji Mifuko 22, Kamati ya Siasa ya Wilaya CCM-Saruji Mifuko 15 na DED na wenzake-Saruji Mifuko 20.

Wengine waliochangia kwenye harambee hiyo ni: “DC na wenzake- Saruji Mifuko 62, Mbunge wa Jimbo hilo la Musoma Vijijini-Saruji Mifuko 200,

Aidha, fedha taslimu,Tsh248,000 (zikiwemo Tsh 105,000 za walimu makada wa CCM).

“Karibuni tujenge Sekondari ya Kisiwa cha Rukuba cha Musoma Vijijini.

Furaha na shauku ya ujenzi wa Sekondari Kisiwani Rukuba ni yetu sote” Imeeleza taarifa hiyo.

Kisiwa cha Rukuba ni moja ya vijiji vinne vya Kata ya Etaro ambapo wanafunzi wa sekondari kutoka Kisiwani humo wanasoma nchi kavu kwenye sekondari ya Kata yao (Etaro Sekondari).

Ambapo imeelezwa kuwa, wanafunzi hao wanakumbana na matatizo mengi ambayo yanadhoofisha maendeleo yao kielimu hivyo wakazi hao wameamua kujenga sekondari yao Kisiwani humo.

By Jamhuri