Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu ya historia ya Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim kwenye bango maalum kabla ya kuzindua Tovuti ya Hifadhi ya Nyaraka za Kumbukumbu za Kidigitali za Kiongozi huyo kutoka kwa mtoto wake wa kiume, Ahmed Salim kwenye hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam tarehe 30 Septemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na wanafamilia wa Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim mara baada ya kuzindua Tovuti ya Hifadhi ya Nyaraka za Kumbukumbu za Kidigitali za Kiongozi huyo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam tarehe 30 Septemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tovuti ya Hifadhi ya Nyaraka za Kumbukumbu za Kidigitali za Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam tarehe 30 Septemba, 2023.

By Jamhuri