Mwanaume wa kwanza kupandikizwa figo iliyobadilishwa vinasaba kutoka kwa nguruwe ameruhusiwa kutoka hospitalini.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 62 aliruhusiwa kwenda nyumbani, wiki mbili baada ya upasuaji wa dharura katika Hospitali Kuu ya Massachusetts (MGH).

Upandikizaji wa viungo kutoka kwa nguruwe waliobadilishwa vinasaba haukufanikiwa siku za nyuma.

Lakini mafanikio ya utaratibu huu hadi sasa yamesifiwa na wanasayansi kama hatua ya kihistoria katika uwanja wa upandikizaji.

Katika taarifa, hospitali ilisema mgonjwa, Richard “Rick” Slayman wa Weymouth, Massachusetts, alikuwa akipambana na ugonjwa wa figo na alihitaji kupandikizwa kiungo hicho ili kuokoa maisha yake.

Madaktari wake walifanikiwa kupandikiza figo ya nguruwe iliyobadilishwa vinasaba katika mwili wake katika upasuaji ulifanyika kwa saa nne tarehe 16 mwezi Machi.

Walisema figo ya Bw Slayman sasa inafanya kazi vizuri na kwamba hahitaji kufanyiwa tiba ya dialysis.

Katika taarifa, Bw Slayman amepokwa kwa furaha uamuzi wa madaktari kumruhusu kuondoka hospitalini.

Ni “mojawapo ya nyakati za furaha” maishani mwake, alisema

By Jamhuri