Na Tatu Saad, JAMHURI MEDIA

Mahakama ya hakimu Mkazi kisutu imewahukumu kifungo Cha miaka mitatu jela wakazi wa Ilala Daresalaam Habibu Ibrahim Habibu (24) na Salumu mashtaka duchi baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya cocaine g60.2

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu Romuli Mbuya mbele ya wakili wa Serikari Faraji Nguka Bada ya watuhumiwa kukiri kosa lao.

Pia mahakama hiyo Imetoa amri kuchukuliwa Kwa dawa hizo za kulevya na kupelekwa katika kitengo maalumu kwaajili ya kuteketezwa.

Inadaiwa kuwa mnamo Desemba 21 mwaka 2020 watuhumiwa wakiwa eneo la bandari ya Daresalaam wakielekea Zanzibar walikuwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya Kokein gram 60.2.

Akitoa hukumu hiyo Mbuya amedai awali katika makubaliano ya washitakiwa na muendesha mashitaka upande wa mashtaka waliiomba mahakama kuwapa washitakiwa adhabu Kali Kwa kuzingaia kosa la usafirishaji wa madawa ya kulevya ni kosa la jinai.

Mbuya ameeleza kuwa upande wa washitakiwa waliiomba  mahakama kuwapa adhabu ndogo wakitoa hoja tatu ambazo ni kukaa mahabusu Kwa muda mrefu pia  waliiomba mahakama iwazingatie kuwa ni kosa la kwanza na walikiri kosa lao.

Pia mshitakiwa wa kwanza Habibu Ibrahim Habibu alidai yeye ni mtoto yatima na alikuwa anasoma kidato Cha tano shule ya iringa na alikuwa akijitegemea kulipa ada hivyo aliamua kujiingiza katika usambazaji wa madawa ya kulevya ili apate ada na aweze kuendelea na masomo yake.

Baada ya madai hayo Mbuya aliieleza kuwa ikizingatiwa Kukaa gerezani Kwa muda mrefu mahakama inaweza kuwapunguzia na pia washitakiwa hao ni mara ya kwanza na suala la kukiri kosa linaonyesha kujutia hivyo mahakama imetumia kigezo hicho kuwapunguzia kifungo ambapo watatumikia kifungo Cha miaka mitatu (3) Kwa Kila mmoja.

By Jamhuri