Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Njombe
Imeelezwa kuwa kiwanda cha kuzalisha mipira ya mikono kinachomilikiwa na Bohari ya Dawa (MSD) kilichopo Idofi, wilayani Makambako mkoani Njombe kimepiga hatua kubwa ambapo kinazalisha mipira ya mikono milioni 86.4 sawa na asilimia 83 4 ya mahitaji ya nchi.
Hayo yameelezwa na Kaimu Meneja wa kiwanda hicho, Shiwa Mushi, wakati akizungumza na waandishi na wahariri waliotembelea kiwanda hicho.
Amesema kuwa kwa ya kiwanda hicho kimeanza uzalishaji tangu Februari 12, mwaka huu baada ya kuzinduliwa rasmi na Makamu wa Rais Philip Mpango Oktoba mwaka jana.
“Kwa sasa kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha jozi (pear) 10,000 kwa siku ambapo hadi sasa tayari tayari kimezalisha jozi milioni 2′ amesema.
Mushi ameaema kuwa kiwanda hicho kinachomililiwa na MSD kupitia kampuni yake tanzu ya MSD Medipham Manufacturing CO LTD, ambayo inamiliki viwanda vingine viwili ambavyo vipo hatua za mwisho.
Viwanda hivyo ni kiwanda cha kuzalisha bidhaa za pamba kilichopo Simiyu na Zengereni cha Pwani ambacho kitakuwa kinazalisha dawa.
Etty Kusiruka ni Meneja Mawasiliano na Uhusiano MSD, amesema tayari wanaelekea kuanza kuuza bidhaa zake kwa vituo mbalimbali vya afya vikiwemo vya Serikali na binafsi.
Awali amesema kabla ya kuanzishwa kwa kiwanda hicho, MSD ilikuwa mdau mkubwa wa kununua bidhaa za afya, kuuza na kuzisamba kwa wadau, ikiwemo hosptali, vituo na zanahati.