NA MTANDAO

Morocco imewasilisha rasmi maombi ya kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2026, huku tayari ikiwa imezindua kampeni ya kuandaa michuano hiyo.

Ikumbukwe kuwa hiyo haitakuwa mara ya kwanza kwa taifa hilo la Afrika Kaskazini kuomba kuwa mwenyeji wa mashindano hayo makubwa; kwa mara ya kwanza liliwasilisha maombi yake mwaka 1994, 1998, 2006 na 2010.

Mwenyekiti wa kampeni hiyo, Moulay hafidh Elalamy, amesema nchi yake iko tayari kulibeba jukumu hilo na kuongeza kuwa litakuwa jambo jema na lenye manufaa kwa Bara la Afrika endapo nchi yake itafanikiwa kuwa mwenyeji wa michuano hiyo.

Amesema endapo nchi yake itapewa wenyeji wa michuano hiyo, wanatarajia kupata ufanisi wa kibiashara na kuacha historia kubwa nchini humo na ndani ya Afrika na duniani yote ya wapenda mchezo wa soka kwa ujumla.

Morocco inataka kubadili hayo yote na imemteua Elalamy, Waziri wa Serikali, kuongoza ombi hilo huku aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika, Hicham El Amrani, akiwa Ofisa Mtendaji Mkuu.

Mwaka 2010, mashindano ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza yalifanyika katika ardhi ya Afrika nchini Afrika Kusini, hata hivyo uamuzi wa  nani atakayeandaa kombe hilo unatarajiwa kufanyika Juni 13 mwaka huu katika Mji wa Moscow nchini Urusi.

Je, Afrika itapata nafasi nyingine ya kuandaa michuano ya kombe hili? Hilo ni swali ambalo majibu yake yatategemeana na uamuzi utakaotolewa.

Mwisho.

Please follow and like us:
Pin Share