Mama wa mtoto mwenye umri wa miaka mitano ambaye alinusurika kifo baada ya kumeza vyuma 52 kutoka kwenye kifaa cha kuchezea amewatahadharisha wazazi kutambua hatari iliyomkumba mtoto.

Daktari alilazimika kupasua tumbo la mtoto Jude sehemu tano ili kuondoa vyuma vilivyokua vimekwama tumboni mwake .

Mama wa mtoto huyo Lyndsey Foley amesema alihofia kuwa mtoto wake angefariki.

Wizara ya Afya ya Wales (PHW) imewatoa wito kwa watu kuwa makini na kufikiria kabla ya kununua bidhaa kwa ajili ya watoto wao zenye vyuma vidogo na betri na vifungo.

Foley, 34, amesema alianza kuwa na wasiwasi baada ya mtoto wake kushindwa kupona baada ya kuugua kwa wiki kadhaa.

Baada ya kuongezeka kwa wasiwasi,Agosti alimpeleka Jude katika hospitali ya Prince Charles akiwa na maumivu makali.

Uchunguzi na kipimo cha X-Ray vilibaini kuwa alikuwa na vyuma tumboni.