Mufti atengua uteuzi wa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam

Baraza la Ulamaa katlika kikao chake ilichofanyika tarehe O1 na 2 Februari jjini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dr. Abubakar Zubeir bin Ally LIMETENGUA uteuzi wa Sheikh Alhad Mussa Salum kama Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam kuanzia leo tarehe 2 Februari 2023.


Wakati huo huo Mheshimiwa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dr. Abubakar Zubeir bin Ally AMEMTEUA Shelkh Walid Alhad Omar kukaimu nafasi ya Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam kuanzia leo tarehe 2 February 2023.