Hospitali ya Taifa Muhimbili imepokea msaada wa viti mwendo 21 vyenye thamani ya TZS. 5.7Mil kutoka kampuni ya Stufit Afrika PVT. Ltd kwa lengo la kusaidia wagonjwa mbalimbali wanaokuja hospitalini hapo.

Akipokea msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi ameshukuru kampuni hiyo kwa msaada huo ambao utasaidia wagonjwa wanaohitaji usaidizi kutoka sehemu moja hadi nyingine.

” Tunashukuru kampuni ya Stufit Afrika PVT. Ltd kwa kuguswa na kuona uhitaji huu kwa wagonjwa ambao wengi wao ni Watanzania wenzetu ambao wanapitia changamoto mbalimbali za afya, kwani uhitaji ni mkubwa kulingana na wagonjwa tunaowahudumia,” ameongeza Prof. Janabi