Na Cresensia Kapinga,JamhuriMedia,Songea

Naibu Waziri wa maji mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka wakazi wa manispaa ya Songea na vitongoji vyake kuona umuhimu wa kutunza mazingira kwenye vyanzo vya maji ili miradi ya maji inayotekelezwa na serikali iweze kuwa endelevu pamoja na kuhakikisha miundombinu ya maji safi na usafi wa mazingira inalindwa kwakuwa maji ni rasilimali muhimu inayogusa maisha ya kila kiumbe.

Naibu Waziri huyo ameyasema hayo jana kwenye hafla fupi ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa miji 28 katika mji wa Songea wenye thamani ya sh. Bilioni 145.7 iliyofanyika kwenye eneo la viwanja vya Matarawe Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma na mkandarasi wa china Civil Engineering Construction Corporation (CCECC).

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira (SOUWASA),akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa miji 28 katika mji wa Songea wenye thamani ya sh. Bilioni 145.7 iliyofanyika kwenye eneo la viwanja vya Matarawe Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Amesema kuwa jamii na mazingira ni maswala yanayoshabiiana, vile vile hali ya umaskini inasababisha uharibufu wa vyanzo vya maji hivyo kwa kutambua hilo serikali inachukuwa hatua mbalimbali za uhifadhi wa mazingira kama vile utungaji wa sera ya Taifa ya mazingira ya mwaka 1997, Sheria ya mazingira namba 20 ya mwaka 2004 na mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Amesema kuwa kuongezeka kwa idadi ya watu imekuwa sababu ya uharibufu wa mazingira lakini selikari inaendelea kutoa elimu na kuhakikisha wanapeleka miongozo, Sheria ,kanuni zitakazo fuatwa ili kuwa walinzi na watunzaji wa mazingira na hatimae watunzaji wa vyanzo vya maji.

“Kukua kwa shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo cha mabondeni,kuchunga mifugo,kuchoma misitu moto vinachangia uchafuzi wa vyanzo vya maji na uhaba mkubwa wa maji na ili kuepuka janga hili linaloashiria kutokea siku za usoni la uhaba mkubwa wa maji hatuna budi kutumia nguvu zetu zote kuzuia janga hilo kwa kutoa elimu itakayomfanya kila mmoja wetu kuona kuwa anao wajibu mkubwa wa kutunza mazingira ili vyanzo vyetu vya maji viwe endelevu.”amesema mhandisi Mahundi.

Amesema kuwa kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi iliyofanyika 2022 matokeo ya awali yanaonesha kuwa Mkoa wa Ruvuma unakadiliwa kuwa na wakazi wapatao milioni 1.8 na Manispaa ya Songea na vitongoji vyake vinawakazi wapatao laki 286,285 ambapo kwa Sasa mahitaji ya maji katika eneo la huduma ni wastani wa lita milioni 20.33 kwa siku ambazo ni matumizi ya majumbani ,viwandani,biashara na taasisi.

“Sisi kama wizara ya maji ili kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji katika mji wa Songea serikali kupitia mradi wa maji wa miji 28 utaongeza kiwango cha kuzalisha maji kwa kiasi cha lita milioni 31,000 kwa siku na hii ni kupitia taarifa ya upembuzi yakinifu wa kienolojia na upembuzi yakinifu wa kiaidrojia za ujenzi wa bwawa utaonesha kuwa bwawa litakalojengwa litakuwa na uwezo wa kuhifadi maji kiasi cha lita bilioni 4.8” amesema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Injinia Nadhifa Kemikimba amesema kuwa mradi huo utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuhudumia wananchi wa Songea hadi mwaka 2045 ambapo idadi ya watu ya wakazi wa Songea inatarajiwa kuwa zaidi ya laki 4.

Naibu Waziri wa maji mhandisi Maryprisca Mahundi akiwa ameongozana ka Katibu Wkuu wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba pamoja na mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas wakiwasili viwanja vya matarawe Manispaa ya Songea tayari kwa utiaji sahihi mkataba wa mradi wa maji wenye thamani ya sh. Bilioni 145.7

Injinia Kemikimba amezitaja kazi zitakazo fanyika kwenye mradi huo kuwa ni ujenzi wa bwawa lenye uwezo wa kujaza maji lita milioni 16 kwa siku, ujenzi wa matenki 10 yatakayosafilisha maji kutoka kwenye bwawa hadi kwenye matenki pia usambazaji wa maji wenye kilometa zaidi ya laki 4.

Awali akisoma taarifa ya mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (SOUWASA) Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Mhandisi Patrick Kibasa kwa mgeni rasmi naibu Waziri wa maji mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye amemuwakilisha Waziri wa maji Juma aweso, amemshuku rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia suluhu pamoja na wizara ya maji kwa kwa kutoa fedha hizo kiasi cha sh.bilioni 145.7 ambazo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuondokana na tatizo la maji katika Manispaa ya Songea.

Ametaja changamoto kubwa ya utiaji wa huduma ya maji safi katika Manispaa ya Songea ni uwezo mdogo wa kuzalisha maji dhidi ya mahitaji , mamlaka inauwezo wa kuzalisha lita milioni 11.58 kwa siku dhidi ya mahitaji ya lita milioni 20 .33 kwa siku.

Mhandisi Kibasa amesema kuwa mahitaji makubwa ni ya nishati ya umeme ambao mamlaka inatumia wastani wa sh milioni 32 kwa mwezi ili kusukuma maji kwenda kwa wateja .

By Jamhuri