Netanyahu ameongeza kwamba bila ya operesheni kubwa za kijeshi zilizofanywa kwa pamoja na Marekani basi huenda Iran ingekuwa tayari inayo mabomu ya nyuklia na mamilioni ya Waisrael sasa wangekabiliwa na vitisho.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kampeni ya kijeshi ya Israel dhidi ya Iran imefanikiwa kuizuia nchi hiyo kupata silaha za nyuklia na kwamba wamekiondoa kitisho kilichokuwepo dhidi yao.
Netanyahu ameongeza kwamba bila ya operesheni kubwa za kijeshi zilizofanywa kwa pamoja na Marekani basi huenda Iran ingekuwa tayari inayo mabomu ya nyuklia na mamilioni ya Waisrael sasa wangekabiliwa na vitisho kutoka kwa taifa hilo la Jamhuri ya Kiislam.
Lakini mara zote Iran imeyakanusha madai hayo na kwamba mpango wake wa nyuklia unakusudiwa kwa madhumuni ya kiraia pekee.
Hata hivyo, licha ya makubaliano ya amani yaliyofikiwa kati ya Marekani na Iran,Israel yenyewe imesema kampeni yake dhidi ya Iran na washirika wake bado inaendelea. Vikosi vyake vitasalia katika maeneo yenye usalama nchini Lebanon, Syria na Ukanda wa Gaza bila ukomo wa muda.


