Papa Benedict wa XVI afariki Dunia akiwa na umri wa miaka 95

Papa Benedict wa XVI amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 katika makazi yake huko Vatican Roma.

Vatican imetangaza kifo hicho kupitia mitandao ya kijamii leo Desemba 31, 2022 na kusema kuwa taarifa na ufafanuzi kamili utatolewa hapo baadaye.

Mapema wiki hii Papa Francis alipokuwa akihutubia alisema kuwa hali ya Papa Benedicto VXI sio nzuri na hivyo kuwataka mahujaji kumuombea.

Papa Benedicto wa VXI aliyezaliwa mwaka 1927 ameliongoza kanisa la Khatholic kuanzia mwaka 2005 hadi 2013 alipojiuzuru wadhifa huo.