Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia,Dodoma

MAMLAKA ya Udhibiti wa ununuzi wa Umma (PPRA)kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais (TAMISEMI)wameandaa semina kazi kwa ajili ya kuhakikisha wakurugenzi wanazingatia sheria za manunuzi kupitia Mfumo wa ununuzi wa Umma wa kielektroniki ujulikanao kama NeST ili kudhibiti ununuzi wa Umma unaozingatia uwazi.

Mfumo huo wa NeST unatarajiwa kutatua changamoto za kiufundi katika manunuzi na hivyo kukidhi mahitaji ya Serikali Katika Sekta ya manunuzi.

Akizungumza kwenye semina hiyo leo November 23,2023 jijini Dodoma Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia Serikali za mitaa na Tawala za Mikoa Sospita Mtwale ameeleza kuwa Mfumo huo utasaidia Serikali za mitaa na halmashauri zote nchiniili kufanya manunuzi kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuendana na Mamlaka ya Serikali mtandao inayoelekeza matumizi na manunuzi yote ya serikali kufanywa kidigitali.

“Nitoe rai kwa Wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanazingatia maelekezo ya PPRA kwa ufasaha ,watakaokiuka tulishatoa maelekezo kwa mujibi wa sheria ya PPRA kuwafikisha mahakamani,tuna imani semina hii itasaidia wakutugenzi kurudi kwenye mstari Manunuzi yote lazima yafuate utaratibu wa serikali, “amesema

Eliakim Maswi, Afisa Mtendaji Mkuu PPRA

Amesema Serikali imekuwa ikiboresha mifumo ya manunuzi mara kwa mara kuendana na mabadiliko ya kidunia ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo(PPRA)Eliakim Maswi ameeleza kuwa licha ya kuutambulisha mfumo huo mwitikio bado hauridhishi kutokana na baadhi ya Halmashauri kushindwa kuutumia .

Amesema kati ya Halmashauri zote 184 nchini ni Halmashauri sita tu ambazo sawa na asilimia 3.3 ya Halmashauri zote ndizo ambazo zimeanza kutumia Mfumo huo mpya wa Kielektronic NeST na kufafanua kuwa Halmashauri za Miji zikiwemo za Dar es salaam, Mwanza, Mbeya hazijawai kabisa kutumia Mfumo huo.

“Ni muhimu kwa wakurugenzi kutumia mfumo huu, lengo ni wajengea uwezo wakurugenzi wa Halmashauri Juu ya umuhimu wa kutumia Mfumo mpya wa ununuzi wa Umma ambapo Halmashauri 115 hazina habari kama kunakutumia mfumo, ” Ameeleza

Maswi amesema kwa Halmashauri ambazo hazitaki kutumia Mfumo huo wataadhibiwa kwa kitendo cha kutotumia mfumo kwani wanakiuka taratibu na Sheria zilizowekwa ambapo ametaja Halmashauri zilizofanya vizuri kwa kutumia Mfumo kuwa ni pamoja na Ngara ambayo imeweza kukusanya zabuni nyingi ikifuatiwa na Nyanghwale,Misenyi na Makete zabuni .

“Moja ya kuwa nguzo muhimu kwenye NeST ni kuwa na uwezo wa kusajili watumiaji Kwa haraka,urahisi na kwa usahihi, watumiaji watatakiwa kujisajili na kuweka taarifa zinazotakiwa kutokana na aina ya shughuli anayopanga kuifanya kwa kutumia mfumo mara moja tu,”amesema.

Sambamba na hayo alitaja baadhi ya faida zitakazopatikana baada ya kuanza kutumika Kwa mfumo wa NeST kuwa ni kuongezeka Kwa uwazi na kuondoa mwingiliano wa kibinadamu na kuongeza uwajibikaji.

By Jamhuri