Rais ateua wajumbe wa Tume ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameteua Wajumbe wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai nchini inayoongozwa na Mwenyekiti Mhe. Jaji Mohamed Othman Chande na Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Ombeni Yohana Sefue kama ifuatavyo:-

  • Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali;
  • Laurean Philomena Ndumbaro, Katibu Mkuu, UTUMISHI;
  • Said Ally Mwema, Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu;
  • Balozi Ernest Jumbe Mangu, Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu;
  • Edward Gamaya Hoseah, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika;
  • Saada Ibrahim Makungu, Askari Polisi Mstaafu;
  • Omar Issa, Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO;
  • Baraka Leonard, Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais; na
  • Yahya Khamis Hamad, Mkurugenzi wa Utafiti katika Chuo Kikuu cha Zanzibar na Rais Mstaafu wa Chama cha Wanasheria Zanzibar.

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu