Na Mussa Augustine,JamhuriMedia,Dar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Nishati Kuunda kikosi kazi kitakachoshughulikia sera za nishati mbadala ili kufikia malengo ya serikali yakutumia nishati safi ya kupikia.

Raisi Samia ametoa agizo hilo leo Novemba 1, 2022, jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mjadala wa kitaifa wa siku mbili wa kujadili matumizi ya nishati safi ili kuepukana nammadhara yatokanayo na matumizi ya nishati chafu.

Aidha amesema kuwa kikosi kazi hicho kitaongozwa na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa na kitahusisha Wizara mbalimbali zinazohisika katika utunzaji wa mazingira ikiwemo Wizara ya Nishati, TAMISEMI,Wizara ya Muungano na Mazingira ,Wizara ya Afya,Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge na Uratibu na Makundi Maalumu pamoja na sekta binafsi.

Amesema kuwa kikosi hicho kitakua na kazi kubwa ya kuchakata sera nakuja na afua zitakazosaidia kuandaa sera na sheria zitakazowezesha kusimamia matumizi safi,salama na endelevu ya nishati ya kupikia ,ambapo amebainisha kuwa kufikia mwaka 2032 angalau asilimia 80 hadi 90 ya watanzania wawe wanatumia nishati mbadala nakuondokana na madhara yatokanayo na matumizi ya ya nishati chafu yakiwemo madhara ya kiafya na kimazingira .

Rais Samia amesema serikali katika mwaka wa fedha 2023 / 2024 inatarajia kutenga fedha ya kutunisha mfuko wa nishati safi ili kuweza kuwa na rasilimari fedha kwa ajili ya kuwezesha watanzania waishio kwenye mazingira magumu waweze kutumia nishati safi nakuachana na utumiaji wa mkaa na kuni ambao umekuwa ukisababisha ukataji holela wa misitu.

Kwa upande wake Waziri wa Nishati, Januari Makamba, amesema kuwa nishati ya kupikia inatumika kila nyumba hivyo suala hili linapaswa kuchukuliwa kwa uzito wake nakuweza kufikia malengo ya serikali yakuondoa changamoto za gharama zitokanazo na matumizi ya nishati chafu.

“Mheshiniwa rais nishati safi inaweza kubadilisha maisha ya watanzania kutokana na matuzmizi safi,kupika huku unatoa machozi,kamasi ,unakohoa sio jambo zuri ,kupika ni furaha ,hivyo matumizi ya nishati safi tutaokoa afya za watanzania,pia watoto wanaoshindwa kufikia ndoto zao kielemu kutokana na kazi za kutafuta kuni.” amesema Makamba.

Naye Profesa Tubaijuka ameishauri Serikali kuhakikisha inangalia namna ya kupunguza gharama ya gesi,ambapo amebainisha kwamba nishati hiyo imepanda kutoka bei ya awali 18000 nakufikia 24000 hali ambayo kwa mtanzania wa maisha ya kawaida hawezi kumudu gharama hizo.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Mfumo wa Upumuaji Hospitali ya Taifa Muhimbili ,Dkt. Pauline Chale amesema kwamba Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imekuwa imekuwa ikihudumia wagonjwa 60 kwa siku ambapo miongoni mwao ni wale waliopatwa na madhara ya nishati chafu hivyo elimu ya kubadilisha mtazamo wa Watanzania kuacha kutumia nishati chafu inahitajika kwa haraka.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wadau mbalimbali kwenye mabanda ya maonesho kuhusu matumizi ya Nishati safi ya kupikia kabla ya kufungua Kongamano la Kitaifa kuhusu Nishati hiyo lililofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Novemba, 2022.

Mkutano huo wa siku mbili umewakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo ,pamoja na taasisi za Serikali na zisizo za kiserikali kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini, ikiwa lengo ni kujadili namna yakutoka katika matumizi ya nishati chafu nakuhamia katika matumizi ya nishati safi,salama na endelevu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Viongozi pamoja na Wananchi waliohudhuria kwenye Kongamano la Kitaifa kuhusu Nishati Safi ya Kupikia katika ukumbi wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Novemba, 2022.

By Jamhuri