Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa Taasisi mbalimbali, Wanafunzi pamoja na Wananchi wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika yaliyofanyika katika ukumbi wa Nyasa uliopo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha tarehe 11 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna wa Polisi (CP) Salum Hamduni kuhusiana na kazi mbalimbali ambazo Taasisi hiyo inafanya kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika yaliyofanyika katika ukumbi wa Nyasa uliopo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha tarehe 11 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Kamishna wa Uhifadhi TANAPA William Mwakilema wakati alipotembelea Banda la Taasisi hiyo kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika yaliyofanyika katika ukumbi wa Nyasa uliopo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha tarehe 11 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya maua kutoka kwa Kiongozi wa Girl Guide wa Arusha Annasia Vincent Cosmas mara baada ya kuwasili kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika tarehe 11 Julai, 2023.
Viongozi wa Dini, Maafisa kutoka Taasisi mbalimbali, Wanafunzi pamoja na Wananchi wakiwa kwenye ukumbi wa Nyasa uliopo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha kwa ajili ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika tarehe 11 Julai, 2023.
 
Wasanii wa Kikundi cha ngoma za asili kutoka Zanzibar Kibati wakitumbuiza kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika tarehe 11 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo kutoka Bodi ya Ushauri ya Kupambana na Rushwa Afrika iliyowasilishwa na Makamu Mwenyekiti wa AUABC Mhe. Pascoal Antonio Joaquim wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika yaliyofanyika katika ukumbi wa Nyasa uliopo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha tarehe 11 Julai, 2023.

By Jamhuri