Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi wakati akiwasili kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba Mkoani Kagera kwa ajili ya kushiriki Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo Kitaifa yamefanyika Mkoani humo tarehe 14 Oktoba, 2022.
Vijana wa Halaiki wakitumbuiza kwa kuonesha kazi mbalimbali katika Kilele cha Maadhimisho ya Mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo yamefanyika kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba Mkoani Kagera tarehe 14 Oktoba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa vyeti kwa wakimbiza mwenge Kitaifa katika kilele cha mbio za Mwenge mkoani Kagera tarehe 14 Oktoba, 2022.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba Mkoani Kagera kwenye Maadhimisho ya Kilele cha Maadhimisho ya mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo yamefanyika kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba Mkoani Kagera tarehe 14 Oktoba, 2022.