Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Songea

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ruvuma limetoa elimu kwa wananchi wa Kitongoji cha Kisendema kilichopo Kata ya Msisima, Wilaya ya Namtumbo, kuhusu umuhimu wa kulinda miundombinu ya umeme ili kuhakikisha huduma hiyo inaendelea kupatikana kwa uhakika.

Akizungumza Jana wakati wa zoezi hilo, Afisa uhusiano na huduma kwa wateja TANESCO Mkoa wa Ruvuma,Allan Njiro amewataka wananchi kuwa walinzi wa miundombinu ya umeme kwa kutoa taarifa za haraka kuhusu vitendo vya uharibifu, wizi wa nyaya za kwenye Transfoma aina ya copa ,mafuta ya transfoma na vifaa vingine vya umeme vinavyoweza kuhatarisha ukosekanaji wa upatikanaji wa huduma hiyo ya umeme.

TANESCO imekuwa ikiendesha kampeni za kutoa elimu katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu matumizi salama ya umeme na utunzaji wa miundombinu yake.

Aidha, wananchi walikumbushwa kuepuka kufanya shughuli zinazoweza kuhatarisha miundombinu ya umeme na kushirikiana na mamlaka husika katika kuhakikisha uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika sekta ya umeme unalindwa kwa manufaa ya jamii na maendeleo ya kiuchumi nchini.

Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO, Mkoa wa Ruvuma, Allan Njiro akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Kisendema kata ya msimama wilayani Namtumbo.