Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Dkt. Peter Mathuki Hati ya Umiliki wa Ardhi yenye ukubwa wa ekari 125 bure bila malipo yoyote kwa ajili ya Jumuiya hiyo mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Ndogo ya Arusha tarehe 03 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) John Bosco Kalisa Hati ya umiliki wa Ardhi yenye ukubwa wa ekari 3 bure bila malipo yoyote
kwa ajili ya Baraza hilo Jijini Arusha tarehe 03 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mwanachama Mkazi wa Baraza la Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki (EALS) Moses Mahuna Hati ya umiliki wa Ardhi yenye ukubwa wa ekari 5 bure kwa
ajili ya matumizi ya Chama hicho cha Wanasheria kwenye hafla fupi
iliyofanyika Ikulu Ndogo ya Arusha tarehe 03 Machi, 202
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Dkt. Peter Mathuki wanne kutoka (kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax watano kutoka (kulia), Mwakilishi kutoka Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki (EALS) Moses Mahuna watatu kutoka (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) John Bosco Kalisa wanne kutoka (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella watatu kutoka (kulia) pamoja na Katibu Mtendaji wa Chama cha Udhibiti wa Nishati kwa Afrika Mashariki Geoffrey Mabea wa kwanza (kulia) kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Ndogo ya Arusha tarehe 03 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Balozi Mbarouk
Nassoro Mbarouk mara baada ya kukabidhi Hati ya Umiliki wa Ardhi kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika Ikulu Ndogo ya
Arusha tarehe 03 Machi, 2023.

By Jamhuri