RAIS Dk. Samia Dk Samia Suluhu Hassan ameridhishwa na mabadiliko yanayoendelea Bohari ya Dawa ( MSD) na kuwataka waendeleee kuchapa kazi.

Rais Samia amesema hayo leo Jumamosi Agosti 19, 2023 mkoani Arusha wakati akifungua kikao kazi cha wenyeviti wa bodi na taasisi za umma.

Rais Dk.Samia akiwa amemsiamamisha Mkurugenzi wa MSD, Mavere Tukai amesema taasisi hiyo ni kati ya mashirika yaliyibadilika na matumaini yake itakwenda kufanya vizuri hasa katika mfumo wa uuzaji wa Dawa Afrika kwa kuwa na soko kubwa hususani kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC).