Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa venyeviti wa bodi mbalimbali

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya mawasiliano ya Rais ikulu leo Novemba 18, 2023 imeeleza kuwa;

Rais Samia amemteua Mwamini Juma Malemi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jami (NSSF). Bi. Malemi ni Naibu Katibu Mkuu Mstaafu.

Pia amemteua Prof. Yunus Daud Mgaya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana ya Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka. Prof. Mgaya ni Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).

Amemteua Bw. James Bakinege Mbalwe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT) kwa kipindi cha pili.