Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali kuwahimiza waumini wa dini zao kuzingatia mila, utamaduni na maadili ya Kitanzania. 

Rais Samia ametoa wito huo leo katika hafla ya Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 50 ya Kazi ya Utume na Huduma ya Kanisa la Waadventista wa Sabato yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.

Aidha, Rais Samia amewataka Viongozi wa dini kuendelea kuwaandaa watoto na vijana katika malezi yenye maadili na tabia njema ambayo yatawajenga kuwa wazalendo kwa nchi yao.

Serikali inatambua mchango wa Waadventista wa Sabato katika kuelimisha jamii katika ngazi zote kuhusu masuala ya afya na maisha bora kupitia machapisho mbalimbali na vyombo vya habari. 

Vile vile, Rais Samia amewataka viongozi wa dini kuliombea taifa ili liendelee kudumu katika amani, umoja na mshikamano ambayo ndio msingi mkuu wa utekelezaji wa dhamira ya Serikali ya kuwaletea Watanzania maendeleo. 

Kwa upande mwingine, Rais Samia ametoa wito kwa viongozi wa dini kuwaelimisha wananchi kutunza mazingira kwa kupanda miti kwa wingi, kutunza misitu pamoja na vyanzo vya maji ili tabianchi irudi kuwa kama zamani.

…………………………………..

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kuhusu  mradi wa Ujenzi wa Kanisa Jipya la Waadventista wa Sabato katika eneo la Uhindini Jijini Dodoma 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na kuagana na Waumini wa Kanisa la Waadventista wa Sabato pamoja na Wananchi baada ya kukagyua mradi wa Ujenzi wa Kanisa Jipya la Waadventista wa Sabato katika eneo la Uhindini Jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na Waumini wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, kwenye Maadhimisho ya Jubilee ya miaka 50 ya kazi ya Utume na Huduma ya Kanisa la Waadventista wa Sabato yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiondoa kitambaa kama ishara ya kuzindua rasmi Mnara wa kumbukumbu ya Jubilee ya miaka 50 ya Utume na Huduma za Jami Dodoma, wakati wa Maadhimisho ya Jubilee ya miaka 50 ya kazi ya Utume na Huduma ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania, Jimbo la kati mwa Tanzania, yaliyofanyika Uhindini kati SDA Jijini Dodoma 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, akiwa katika Picha ya pamoja wakati wa Maadhimisho ya Jubilee ya miaka 50 ya kazi ya Utume na Huduma ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania,  Jimbo la kati mwa Tanzania, yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato pamoja na Viongozi wengine, alipowasili katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma kwa ajili ya kuhudhuria Maadhimisho ya Jubilee ya miaka 50 ya kazi ya Utume na Huduma ya Jamii katika Kanisa la Waadventista wa Sabato Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania, Jimbo la kati mwa Tanzania

By Jamhuri