Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakiomba Dua wakati wakitoa Heshima za mwisho kwenye Jeneza lenye Mwili wa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi katika uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar tarehe 02 Machi 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa kuaga Mwili wa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi katika uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar tarehe 02 Machi 2024.
Makamu wa Rais wa Namibia Mhe. Netumbo Nandi Ndaitwah akizungumza na waombolezaji wakati wa kuaga Mwili wa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi katika uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar tarehe 02 Machi 2024.
Wananchi waliohudhurua katika uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar kwa ajili ya kutoa Heshima za mwisho kwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyefariki dunia tarehe 29 Februari 2024 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa akipata matibabu ya Saratani ya Mapafu, ambapo anatarajiwa kuzikwa Kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 02 Machi 2024.
Famili ya Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi ikiwa katika uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar kwa ajili ya kutoa Heshima za mwisho kwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyefariki dunia tarehe 29 Februari 2024 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa akipata matibabu ya Saratani ya Mapafu, ambapo anatarajiwa kuzikwa Kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 02 Machi 2024.

By Jamhuri