Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia Maji mara baada ya kuzindua mradi wa Maji Kizimkazi tarehe 29 Agosti, 2023 katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Maji Kizimkazi katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi (hawaonekani pichani) mara baada ya kuzindua mradi wa Maji wa Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya ufunguzi wa hoteli ya Kitalii iitwayo Kwanza iliyopo Kizimkazi Zanzibar Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar tarehe 29 Agosti, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wakati akivuta kitambaa kuzindua ukarabati wa Madarasa 11, Ofisi za Walimu pamoja na Maabara ya Tehama katika Skuli ya Msingi Kizimkazi Mkunguni kwa ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF tarehe 29 Agosti, 2023 Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua vyumba vya madarasa vilivyokarabatiwa pamoja na chumba cha Tehama katika Skuli ya Kizimkazi Mkunguni tarehe 29 Agosti, 2023 Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi wengine wakati akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Madarasa ya Skuli ya Kizimkazi Mkunguni mara baada ya ukarabati tarehe 29 Agosti, 2023 Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi.

By Jamhuri